USTAWI WA JAMHURI YETU YA MUUNGANO UKO HATARINI: Taarifa kuhusu Muswada wa Marekibisho ya Sheria Mbalimbali (Miscellaneous Amendments) No. 3 (2020)

USTAWI WA JAMHURI YETU YA MUUNGANO UKO HATARINI: Taarifa kuhusu Muswada wa Marekibisho ya Sheria Mbalimbali (Miscellaneous Amendments) No. 3 (2020)

Posted 2 years ago by admin

Siku ya Alkhamis, Juni 4, Serikali ilichapisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Miscellaneous Amendments No.3 (2020), ikikusudia kurekebisha Sheria 13. Siku ya Ijumaa, Juni 5 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria iliwatangazia wadau kuwa wanakaribishwa kutoa maoni kwa siku tatu kuanzania Ijumaa Juni 5 mpaka Jumapili Juni 7 kabla ya hatua nyingine kuendelea. Muswada huu uliwasilishwa kwa hati ya dharula na hivyo kupelekea zoezi la kukusanya maoni ya wadau kufanyika kwa haraka hata siku za mapumziko mwisho wa wiki.

SKipekee kabisa, marekebisho haya yanayopendekezwa yanagusa kiini cha jamii yetu, hususan dhana ya utawala wa sheria. Soma hapa Taarifa kuhusu Muswada wa Marekibisho ya Sheria Mbalimbali (Miscellaneous Amendments) No. 3 (2020)