
Ufafanuzi Malalamiko ya Wadau dhidi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ni shirika binafsi la kujitolea na la hiari lisilo la kisiasa wala kibiashara lilosajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania mnamo mwaka 1995. Kituo kinataamali jamii yenye haki na usawa. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaendelea bila kutetereka na utekelezaji wake wa majukumu ya kulinda na kutetea haki za binadamu nchini Tanzania. Katika kujituma kwake Kituo kimeendelea kuwafikia watanzania kwa njia mbalimbali na kupitia kazi hizo Kituo kimepata mrejesho wa pongezi na hata malalamiko na tuhuma kadhaa kutoka kwa wadau.
Ili kutii mahitaji ya wadau wake na kukwepa upotoshaji ambao unaweza kusababishwa na kutokuzijibu tuhuma hizo, Kituo kimeona ni vyema kufafanua tuhuma hizo kama ifuatavyo;
Malalamiko ya Wadau dhidi ya LHRC