Uchambuzi wa Kanuni za Sheria ya Usimamizi wa Mazingira za Kupiga Marufuku Mifuko ya Plastiki,

Uchambuzi wa Kanuni za Sheria ya Usimamizi wa Mazingira za Kupiga Marufuku Mifuko ya Plastiki,

Posted 3 years ago by admin

Tanzania imetangaza kupiga marufuku kutengeneza, kusambaza, kutumia au kutunza mifuko ya plastiki kuanzia tarehe 1 Juni mwaka 2019. Katazo hili linafuatia tangazo lililotolewa na Waziri Mkuu na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira. Katazo la mifuko ya plastiki ni utekelezaji wa kifungu cha 230 (2)(f) ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004. Tangazo la katazo la mifuko ya plastiki limeanza utekelezaji kwa kutungwa kwa Kanuni husika za Usimamizi wa Mazingira za Kupiga Marufuku Mifuko ya Plastiki za mwaka 2019. Kanuni hizi zilitangazwa na Waziri wa Ofisi ya Makamu ya Rais Mambo ya Muungano na Mazingira, Mh. Januari Makamba ambazo zimeanza kutumika terehe 1 Juni 2019.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimefanya uchambuzi wa Kanuni hizo kama ilivyoambatanishwa hapa. 

Tafadhali soma na usambaze kwa wengine.