Uchambuzi wa Hotuba za Bajeti zilizowasilishwa Bungeni kwa Mtazamo wa Haki za Binadamu na Mlipuko wa Janga la Corona

Uchambuzi wa Hotuba za Bajeti zilizowasilishwa Bungeni kwa Mtazamo wa Haki za Binadamu na Mlipuko wa Janga la Corona

Posted 2 years ago by admin

Kituo cha Sheria na Haki za Bianadamu (LHRC) tunatoa uchambuzi huu baada ya kupitia hotuba za bajeti zilizozowasilisha katika Bunge la 11 mpaka Mei 6, 2020. Tunaamini kwamba, uchambuzi huu hii iliyochambua hotuba za bajeti zilizo wasilishwa itasaidia kufanya maboresho ya bajeti ya kila wizara pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Taifa itakayo wasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. LHRC tunawapongeza mawaziri na watendaji wote wa wizara kwa maandalizi ya bajeti zilizowasilishwa Bungeni. Pia tunawapongeza wabunge kwa kuchambua na kutoa mapendekezo yao. 

Uchambuzi huu unaweka mapendekezo ya kimkakati kufuatia uwepo wa maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19). Hili limezingatia ukweli kuwa hakuna anayejua janga hili litaisha lini na utaacha madhara makubwa kwa kiasi gani. Hivyo, nchi inawajibu wa kuendelea na juhudi za kupambana na ugonjwa huu pamoja na kuweka mikakati itakayowezesha taifa kuendelea kipindi ambacho shughuli mbalimbali zimepungua kutokana na tishio la ugonjwa huu.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu mepitia bajeti hii kwa kufuata Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21), Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015, Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/21 kama ilivyotumiwa katika hotuba mbalimbali za bajeti zilizowasilishwa Bungeni katika kipindi hiki.

Uchambuzi huu utakuwa wenye manufaa kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na naibu wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mawaziri husika katika sekta zilizotajwa na Wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Soma zaidi hapa.