TAMKO LA KULAANI MAUAJI YA YA ASKARI POLISI MKOANI ARUSHA YALIYOFANYWA NA RAIA

Posted 3 years ago

TAMKO LA KULAANI MAUAJI YA YA ASKARI POLISI MKOANI ARUSHA YALIYOFANYWA NA RAIA

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mauaji ya kikatili yaliyofanywa kwa Askari Polisi wa Kituo kidogo cha Polisi Mbughuni ajulikanae kama PC Damas siku ya tarehe 23/7/2021 wakati akitekeleza majukumu yake. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinalaani kitendo hiki ambacho kimekiuka haki ya kuishi ya PC Damas.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinatoa rai kwa wananchi kuwa ni vyema wananchi wote wafahamu kwamba Askari Polisi wapo kwa mujibu wa sheria na kazi yao kubwa ni kulinda usalama wa raia na mali zao. Siyo jambo la busara kwa wananchi kuwashambulia maaskari wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao kwani kwa kufanya hivyo ni kujaribu kuwaficha wahalifu na hivyo kuchochea ongezeko la vitendo vya uhalifu katika jamii zetu.

Ni matumaini ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwamba Serikali itachukua hatua za makusudi kuhakikisha kwamba aliyefanya tukio ya mauaji ya PC Damas anatafutwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Imetolewa leo Julai 26, 2021

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu

Anna Henga (Wakili)

Mkurugenzi Mtendaji