
Taarifa kwa Umma: Matukio ya Ukiukwaji wa Haki za Kiraia na Kisiasa
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeendelea na ufuatiliaji wa haki za binadamu kwa lengo la kuhakikisha misingi ya haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia inazingatiwa nchini Tanzania. Kwa kipindi cha hivi karibuni Kituo kimebaini ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia hususani Haki za Kiraia na Kisiasa kinyume na ilivyoidhinishwa katika Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa 1966 na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.