Mahakama ya Afrika Mashariki Kusikiliza Maombi ya Kufuta Kusudio la Rufaa ya Serikali kesi ya Sheria ya Huduma za Habari

Mahakama ya Afrika Mashariki Kusikiliza Maombi ya Kufuta Kusudio la Rufaa ya Serikali kesi ya Sheria ya Huduma za Habari

Posted 2 years ago by admin

Mahakama ya Afrika Mashariki kitendo cha rufaa kimepanga kusikiliza maombi ya kufuta kusudio la rufaa lililowekwa na serikali ya Tanzania katika kesi ya Sheria ya Huduma za Habari. Maombi hayo yalifunguliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheri ana Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC). Maombi haya yatasikilizwa Mei 21, 2020 kwa njia ya mtandao (Videoconferencing) mbele ya jopo la majaji wa rufaa ya mahakama ya Afrika Mashariki ambalo litaongozwa na Raisi wa mahakama hiyo Emmanuel Ugirashebuja akisaidiana na Liboire Nkurunzinza, Aaron Ringera, Geoffrey Kiryabwire na Sauda Mjasiri.

Ikumbukwe kuwa tarehe 28 Machi 2019 Mahakama hiyo ilitoa hukumu yake na kusema baadhi ya vifungu vya Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 vinakiuka Mkataba unaoanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuamuru vifutwe. Kwa kutoridhika na uamuzi wa mahakama serikali ya Tanzania ilitoa taarifa ya nia ya kukata rufaa tarehe 11 Aprili 2019 lakini mpaka leo hakuna rufaa iliyokatwa. Kwa mujibu wa kanuni za kuendesha mashauri katika mahakama hiyo serikali ilitakuwa kukata rufaa ndani ya siku 30 toka tarehe ya kuonesha kusudio la kukata rufaa.

 

#SimamiaHaki