Kesi ya Kikatiba inayopinga vikwazo vya maeneo ambayo abiria wa mabasi ya masafa marefu wanaruhusiwa kupanda na kushuka jijini Dar es Salaam

Kesi ya Kikatiba inayopinga vikwazo vya maeneo ambayo abiria wa mabasi ya masafa marefu wanaruhusiwa kupanda na kushuka jijini Dar es Salaam

Posted 9 hours ago

Kesi hii inahusu masharti yanayowalazimisha abiria wa mabasi ya masafa marefu kutumia maeneo maalumu kwa ajili ya kupanda na kushuka, pamoja na vikwazo kwa wamiliki wa mabasi kuanzisha vituo, ofisi au maeneo mengine ya kutoa huduma kwa abiria.

Masharti haya yanatokana na Sheria Ndogo ya Vituo vya Mabasi na Maegesho ya Vyombo vya Moto za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo za Mwaka 2022 (Gazeti la Serikali. Na. 496 ya 2022), pamoja na Kifungu cha 32(3)(e) cha Sheria ya Leseni za Usafirishaji, Sura ya 317. Sheria Ndogo tajwa, miongoni mwa mambo mengine, inataka mabasi ya masafa marefu kutumia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na mizigo na kuanzia safari zote katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli.

Kwa mujibu wa malalamiko yaliyowasilishwa Mahakamani, masharti hayo yanaweza kuwa na athari kwa abiria wanaoishi au kufanya shughuli zao katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam ikiwemo yale nje ya Wilaya ya Ubungo. Abiria hulazimika kusafiri hadi Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi Luis, ili kuanza au kumaliza safari zao, hali inayoweza kuongeza muda, gharama za usafiri na usumbufu, hususan kwa wanaosafiri na mizigo.

Download