
Hotuba ya Jaji Mstaafu Joseph Warioba wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu
Disemba 10, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kiliungana na jamii ya ulimwengu kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu. Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Mstaafu Joseph Warioba.
Maadhimisho haya yaliambatana na kauli mbiu ya Haki ni ‘Maendeleo, Simamia Haki’ – ikiwa na lengo la kuhimiza umuhimu wa kulinda haki za binadamu katika kuchagiza maendeleo na kuonesha kwamba haki za binadamu na maendeleo haviwezi kutenganishwa.
Hotuba ya Mgeni Rasmi, Jaji Mstaafu Warioba ililenga kuonesha umuhimu wa kulinda amani katika kulinda na kudumisha haki za binadamu, ikitaja kwamba amani ni tunda la haki. Mhe. Warioba kupitia hotuba yake ameonesha kusikitishwa na vitendo vinavyochochea vurugu na uvunjifu wa amani vilivyojitokeza katika uchaguzi mkuu wa Oktoba. Mhe. Warioba amewataka wanasiasa kutimiza wajibu wao wa kisiasa kujenga jamii isiyo na ubaguzi wa kisiasa ambao kwa mujibu wake unaweza kuchochea uvunjifu wa amani ambayo imejengwa kwa muda mrefu na kwa juhudi kubwa.
Soma zaidi hotuba ya Mhe. Warioba hapa