
Ufafanuzi wa Kisheria juu ya Sakata la Mwanafunzi Abdul Nondo
Katika kudumisha haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimeendelea kufanya uangalizi wa utendaji kazi wa serikali ili kuhakikisha inatekeleza majukumu yake bila kukiuka misingi ya haki za binadamu na utawala wa sheria.
Mnamo Machi 7, 2018 Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilipata taarifa za kushtusha za kutokuonekana kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) Ndugu Abdul Nondo na kufarijika baada ya kupata taarifa za kupatikana kwake mapema.
Hata hivyo taarifa za shutuma zilizoelekezwa kwa Abdul Nondo kutoka kwa jeshi la Polisi, Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kujisalimisha kwa Jeshi la Polisi huko Iringa zimekishitua Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na kuona ni vyema kufanya kumbushi ya kisheria kwa jeshi la polisi na viongozi hao kwa kukiuka sheria kama inavyofafanuliwa; Soma hapa