
TAARIFA YA UANGALIZI WA UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO JIMBO LA KINONDONI NA SIHA
Katika kufikia maono ya kupata jamii yenye haki na usawa, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimeendelea kufanya ufuatiliaji wa utendaji kazi wa serikali katika kipindi cha uchaguzi mdogo katika majimbo ya Siha na Kinondoni. Mnamo Februari 9, 2018 Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilipata kibali rasmi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa mwangalizi wa uchaguzi katika jimbo la Kinondoni pamoja na Siha.
Katika kutimiza jukumu hilo la kidemokrasia, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimefanya uangalizi tangu zilipoanza kampeni mnamo tarehe 25/01/2018 na wakati wa uchaguzi ambapo katika chaguzi hizo ndogo Chama cha Mapinduzi kilishinda. Hata hivyo Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu kimebaini masuala kadhaa ya ukiukwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa sheria na taratibu zinazoratibu chaguzi kama yalivyofafanuliwa:-