
TAARIFA KWA UMMA: UFAFANUZI WA HOJA ZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) DHIDI YA TAMKO LA ASASI ZA KIRAIA
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimepokea barua Kumb. Na. BA.71/75/01/124 ya tarehe 22 February 2018 kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndugu Kailima Ramadhani na kupitia kwa umakini mkubwa hoja za Tume ya Taifa ya Uchaguzi dhidi ya tamko lililotolewa na umoja wa Asasi Za Kiraia, chini ya Jukwaa la Wakurugenzi wa AZAKI, Februari 21, 2018 kuzungumzia hali ya usalama wa raia, haki za binadamu na utawala wa sheria hapa nchini.
Baada ya kupitia hoja hizo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimetoa ufafanuzi ufuatao: Ufafanuzi wa hoja za Tume ya Taifa ya Uchaguzi dhidi ya LHRC