KESI YA KUPINGA TOZO YAUNGURUMA MAHAKAMANI

KESI YA KUPINGA TOZO YAUNGURUMA MAHAKAMANI

Posted tokea miaka 3

 

TAARIFA KWA UMMA

Kesi ya kupinga tozo ya miamala ya simu iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) shauri la namba 11 la mwaka 2021 imesikilizwa leo kwa mara ya pili saa nne (4) asubuhi mbele ya Mheshimiwa Jaji John Mgeta katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.

Kesi hiyo imesikilizwa ambapo mawakili wa upande wa serikali wameweka mapingamizi yakiomba kuifuta kesi hiyo kwa madai ya kwamba kesi hiyo haina mashiko. Mapingamizi hayo matatu yaliyoletwa na upande wa serikali unadai:

  1. Mahakama kuu haina uwezo wa kutoa nafuu zilizoombwa(untenable)
  2. Madai yamekosa sababu za msingi na

(iii) Madai hayo yamekosa ruhusa ya bodi ya mdai (Board Resolution).

Mahakama imesikiliza mapingamizi hayo ambapo upande wa serikali uliwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali Wakili Gabriel Malata na upande wa mlalamikaji uliwakilishwa na Wakili Mpale Mpoki.

Kesi hiyo imepangwa tena tarehe 08/09/2021 ambapo mahakama itatoa uamuzi kuhusu mapingamizi hayo.

Imetolewa leo Agosti 18, 2021 na;

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)

 

Bi. Anna Henga (Wakili)

Mkurugenzi Mtendaji