Uchambuzi wa LHRC: Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa 2026

Uchambuzi wa LHRC: Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa 2026

Posted 21 hours ago

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimefanya uchambuzi na kuwasilisha maoni yake kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa mwaka 2026, uliochapishwa katika Gazeti Maalum la Serikali Na. 9, Juzuu ya 107 tarehe 5 Juni 2026. Muswada unapendekeza marekebisho ya sheria kuu saba(7). Uchambuzi wa LHRC umejikita katika marekebisho ya sheria tatu (3) yanayogusa moja kwa moja haki za kumiliki mali, utawala wa kikatiba, uhuru wa mahakama na mamlaka ya taifa juu ya rasilimali asilia; a) Marekebisho ya Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (Sura ya 116). b) Marekebisho ya Sheria ya Utajiri wa Asili na Rasilimali (Mamlaka ya Kudumu ya Taifa) (Sura ya 449). c) Marekebisho ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Sura ya 283).

Download