LHRC HQ: Justice Lugakingira House
+255 22 2773038 / +255 22 2773048

Jarida la Mlinzi wa Haki - Januari - Machi 2018

  • Jarida la Mlinzi wa Haki - Januari - Machi 2018

JARIDA LA MLINZI WA HAKI - JANUARI - MACHI 2018


Organization Report

Report attachment

Download

Salaam ndugu msomaji,
Karibu katika toleo rasmi la jarida letu la Mlinzi wa Haki, jarida hili ni la pili tangu kusajiliwa rasmi na kupata leseni ya uchapishaji wa jarida letu. Mlinzi wa Haki ni jarida linalobeba dhana nzima ya kazi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambayo ni utetezi na ulinzi wa haki za binadamu. Toleo hili linajumuisha taarifa ya kazi zilizofanyika katika robo ya kwanza ya mwaka 2018.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu tumeuanza mwaka 2018 tukiwa na ari mpya ya kuendeleza utetezi wa haki za binadamu kwa lengo la kuifikia jamii yenye haki na usawa. Katika kipindi cha Januari hadi Machi Kituo kimefanya shughuli mbalimbali ambazo zina mchango mkubwa katika kuimarisha hali ya haki ya haki za binadamu na utawaa wa sheria nchini. Moja ya matukio makubwa ni pamoja na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambapo Kituo kiliwakutanisha wanawake kutoka katika kada mbalimbali kusheherekea mafanikio ya wanawake sambamba na kuimarisha mikakati ya namna ya kuboresha ustawi wa haki za wanawake nchini Tanzania.

Pia Kituo kiliitisha mdahalo wa uliowakutanisha wadau kutoka sekta kujadili mchango wa katiba katika kuimarisha demokrasia na amani nchini. Kituo pia kimeendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika maendeo tofauti ya nchi ikiewemo Mradi wa Kutokomeza Ukeketaji huko wilayani Serengeti Mara; Mradi wa Kuwezesha Wasichana na Wanawake Wadogo ili Kuiwajibisha Jamii kutoa Huduma bora za Afya ya VVU/UKIMWI mkoani Shinyanga; Mradi wa Kuzuia Ufurutu Aga mkoani Arusha na Tanga; Mradi wa Uwezeshaji wa Kisheria Mijini jijini Dar es Salaam pamoja na Mradi wa Kupanua Ushiriki wa Wananchi. Kituo kimeendelea na shughuli mbalimbali za uchechemuzi ikiwemo utoaji elimu kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kwa ujasiri mkubwa Kituo kimeendelea kukemea vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala wa sheria kwa kuzikumbusha mamlaka na wananchi kufuata sheria na kuheshimu haki za binadamu.

Katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka Kituo kimetoa matamko kukemea ukiukwaji wa haki ya kuishi uliotokea katika maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo mauaji ya kikatili yaliyotoea kwa Godfrey Luena na mwanafunzi Akwilina Akwilini. Kupitia matamko hayo Kituo kimezitaka mamlaka pamoja na wananchi kwa ujumla kuwajibika katika kulinda haki za binadamu. Vile vile Kituo kimeendelea kutoa msaada wa kisheria kwa watanzania wasio na uwezo wa kufikia gharama za haki. Kupitia Kituo cha Mfano cha Msaada wa Kisheria cha Kinondoni pamoja na Kituo cha Msaada wa Kisheria Arusha na pia kupitia huduma za msaada wa kisheria wa kuhama hama LHRC imewasaidia jumla ya watanzania 2,577 (849 Wanawake na1728 Wanaume) kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2018.

Zaidi ya hapo, Kituo kimefungua vituo vinne (4) vipya vya msaada wa kisheria katika kata nne tofauti ambazo ni Somangila na Kibada katika wilaya ya Kigamboni pamoja na Mnyamani na Kitunda katika wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kituo kimefanya mengi kana kwamba ni ngumu kuyaweka kwa ufupi katika ukurasa mmoja.

Furahia kulisoma jarida letu kwa undani ili uweze kufahamu zaidi kuhusu Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na kazi zake. Usisite kutoa maoni kwa kadiri utakavyoona inafaa.

Jarida la Mlinzi wa Haki - Januari - Machi 2018

Wakatabahu,

Dkt. Helen Kijo Bisimba

Mkurugenzi Mtendaji